Brazil: Rais Lula kuchunguzwa kwa tuhuma za ufisadi

Lula ameongoza Brazili kuanzia 2003 mpaka 2011
Image caption Lula ameongoza Brazili kuanzia 2003 mpaka 2011

Mahakama kuu nchini Brazil imesema kuwa Rais wa zamani wa nchi hiyo Luiz Inácio Lula da Silva atachunguzwa ili kuthibitisha kama kweli alihusika katika kashfa ya ufisadi kwenye kampuni kubwa ya mafuta nchini humo Petrobras.

Waendesha mashitaka nchini humo wamesema kuwa Lula alikuwa muhimili mkubwa katika utekelezwaji wa rushwa hiyo.

Lula amekana kuhusika na kusema kuwa hizo ni mbinu za kisiasa za kumzuia kuwania urais mwaka 2018.