Ghasia zazuka katika mazishi Kashmir

Pakistan na India zimezozana kuhusu eneo hilo la Kashmir Haki miliki ya picha AP

Kumekuwa na ghasia Srinagar - mji mkubwa katika eneo la kasmir linalotawaliwa na India - baada ya wanajeshi kufyetua gesi ya kutoa machozi katika mazishi ya mvulana mdogo aliyeuawa katika maandamano ya kupinga utawala wa India.

Kifo cha mvulana huyo mwenye umri wa miaka 12 kimezusha hasira kubwa Srinagar.

Polisi wanasema hakushiriki maandamano hayo lakini alipigwa risasi na kuuawa nje ya nyumbani kwao.

Maelfu wamejitokeza katika mazishi hayo.

Lakini wakaazi wanasema ghasia zimezuka wakati polisi walijaribu kuwasitisha waombolezaji kutoingia katika msafara wa mazishi..

Kumekuwa na wasiwasi katika eneo hilo la Kashmir linalotawalaiwa na India tangu Julai, wakati kiongozi maarufu wa wanamgambo alipouawa na waanjeshi wa India.