Nyoka 'watoroka' katika shamba China

cobra

Maafisa mashariki mwa China wanawasaka zaidi ya nyoka 50 aina ya swila (cobra kwa Kiingereza) waliotoweka kutoka shamba la nyoka linaloendeshwa bila ya kibali .

Zaidi ya nyoka 200 walitoweka kutoka shamba hilo mnamo Agosti mwaka huu. Wafugaji nyoka katika shamba hilo wameambia polisi kwamba walikuwa wanajaribu kuwasaka nyoka hao waliotoroka pasi kuwaarifa maafisa wa eneo hilo.

Tatizo hilo lilidhirika kwa umma baada ya swila mmoja kuonekana na kuwashutusha wakaazi katika shamba jingine kwenye eneo la karibu.

Serikali ya eneo hilo inajaribu kuwahakikishia wakaazi kuwa wana dawa za kutosha za kukata sumu ya nyoka hao iwapo wakaazi wataumwa kabla ya nyoka wote kupatikana.