Waliochoshwa na maisha kusaidiwa kufa Uholanzi

Mikono Haki miliki ya picha Thinkstock

Serikali ya Uholanzi inanuia kutunga sheria itakayo halalisha mpango wa kuwaisaidia watu kujitoa uhai, kwa wanaohisi 'wametimiza maisha kimailifu' na sio kuwa ni wagonjwa wasiotibika, Reuters inaripoti.

Uholanzi ndio nchi ya kwanza kuidhinisha huduma ya kuwaisaidia watu kufa - euthanasia, mnamo 2002, lakini ni kwa wagonjwa wanaooonekana kuteseka kwa magonja yasio na tiba.

Reuters imeripoti, mawaziri wa afya na haki nchini wamesema katika barua ya wazi iliowasilishwa bungeni, muongozo wa kuhusu vipi mpango huo utakavyotekelezwa bado unatarajiwa kushughulikiwa.

Lakini watu wanaojihisi kuwa wameishi maisha kwa kutosheka na kuwa hawataki tena kuwa hai, ni lazima wapewe heshima wanayosathili kwa kuruhusiwa kujitoa uhai ila kwa kufuatwa kikamilifu na kwa umakini muongozo utakaowekwa.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ubelgiji ni moja ya mataifa yanayoruhusu huduma ya kusaidiwa mgonjwa asiyetibika kujitoa uhai.

Huenda pendekezo hilo likawachochea wakosoaji wanaosema mpango wa kutoa usaidizi mgonjwa asiyetibika kujitoa uhai tayari umevuka mipaka iliyopangiwa mpango huo, ambapo sasa kielelezo cha wanaoteseka kupindukia kikitumika siyo tu kwa watu wanaougua magonjwa ytasio tibika bali pia sasa wale walio na matatizo ya akili.

Waziri wa Afya Edith Schippers ameandika katika barua hiyo kuwa " kwasabau ombi la kujitoa uhai sana hutoka kwa watu wazima, mpango huu mpya utakua ni wao tu", Inaripoti Reuters.

Hakueleza ni umri wa kati miaka mingapi hadi mingapi.

Sheria hiyo mpya itahitaji "muongozo wa makini na ukaguzi kabla ya kuidhinishwa, utakao fanywa na mtu anayetoa 'usaidizi wa binaadamu kujitoa uhai' aliyesomea utabibu, ambaye pia ana mafunzo ya ziada."

Kwa mujibu wa Reuters, wanatarajia kuitunga sheria hiyo kwa uhsauri wa madaktari na wataalamu wengine kufikia mwishoni mwa 2017.