Vita dhidi ya itikadi kali Kenya
Huwezi kusikiliza tena

Vita dhidi ya itikadi kali Kenya 'vinashinikiza' misimamo hiyo.

Jitahada za Kenya kumaliza itikadi kali za kidini huenda inashinikiza kuongezeka kwa misimamo hiyo, kulingana na wapiganaji waliorejea kutoka Somalia. Kenya imekabiliwa na mashambulizi makali tangu kuvamia nchi jirani ya Somai. Serikali imejaribu mbinu zote kukabiliana na tatizo hili, kuanzia matumizi ya nguvu nyingi hadi kutoa msamaha. Lakini wakaazi wa pwani wanasema dhulma walizotenda walinda usalama zinawasukuma vijana wengi mikononi mwa watu wenye itikadi kali.

Ferdinand Omondi anaripoti kutoka Mombasa.