Guterres:mgogoro wa Syria ni changamoto kubwa

Antonio Guterres
Image caption Antonio Guterres, ndiye mrithi wa Ban Ki Moon.

Katibu mkuu mpya aliyeteuliwa wa umoja wa mataifa Antonio Guterres, ameonya kuwa dunia sasa inakumbana na matatizo makubwa. Katika mahajiano yake ya kwanza tangu kuteuliwa kwake ameiambia BBC kuwa kumaliza vita nchini Syria ndio changamoto kubwa aliyokuwa nayo.

waziri mkuu huyo wa zamani wa Portuguese amesema mgogoro mkubwa wa dunia ni wa Syria na viongozi wa dunia wanatakiwa kujua kuwa kunatakiwa ushirikiano katika kumaliza vita Syria.

Guterres amesema kuwa ishara ya ushirikiano ya umoja wa mataifa kuchamgua yeye ni alama kuwa nchi zinatakiwa kulenga kutatua migogoro ya dunia kuliko kuangalia maslahi yao binafsi.

mkutano mkuu wa umoja wa mataifa unatarajiwa kuanza wiki ijayo ili kuadhinisha kuteuliwa kwake kwa muda wa miaka mitano ijayo.