Madhila ya wazee pwani ya Kenya
Huwezi kusikiliza tena

Madhila ya wazee pwani ya Kenya

Takriban wazee 20 wanauwawa kila mwezi kwa kisingizio cha kuwa wachawi, lengo likiwa kunyakua mashamba yao ya urithi. Haya ni kulingana na mashirika ya kijamii na ripoti za polisi. Haya yanajiri wakati pwani ya Kenya inaendelea kukua kwa kasi kiuchumi kutokana na miradi ya mabilioni ya dola inayozinduliwa na upatikanaji wa madini. Hata hivyo filamu moja ya uhalisia inalenga kumaliza unyama huo, kwa kutoa simulizi ya uhalisia kupitia kwa sauti za waathirika halisi.

Anthony Irungu ana taarifa Zaidi.