'Kadi ya njano' kwa rais Kabila
Huwezi kusikiliza tena

'Kadi ya njano' kwa rais Kabila

Wapinzani wa vyama vya kisiasa katika Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo wamedhamiria kuandamana ili kuweka shinikizo kwa rais Kabila akubali kukaa meza moja pamoja nao kwa mazungumzo na aachilie madaraka ifikapo tarehe kumi na tisa Desemba mwaka huu.

Raia wametakiwa kujiunga kwa kutokwenda kazini, na kuyaita maandamano hayo 'kadi ya njano' kwa rais huyo asiyetaka kuachilia madaraka.

Mbelechi Msochi anaarifu zaidi