Brazil: Spika wa bunge akamatwa kwa tuhuma za rushwa

Amekuwa mmoja wa viongozi wa kisiasa wenye nguvu kubwa kwa miaka mingi
Image caption Amekuwa mmoja wa viongozi wa kisiasa wenye nguvu kubwa kwa miaka mingi

Spika wa zamani wa bunge la Brazil, Edwardo Cunha amekamatwa akihusishwa na rushwa.

Bwana Cunha alituhumiwa kwa kuchukuwa dola milioni tano kama hongo kutoka kwa kampuni ambayo ilishinda mikataba na kampuni ya mafuta ya serikali, Petrobras.

Amekuwa mmoja wa viongozi wa kisiasa wenye nguvu kubwa kwa miaka mingi.

Aliongoza mashtaka dhidi ya aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Dilma Rousseff, ambaye aliondolewa madarakani mwezi Agosti.

Image caption Eduardo Cunha alijiuzulu katika wadhifa wake mwezi Julai 2016

Cunha aliondolewa kutoka bunge la Brazil mwezi uliopita kwa kudanganya kuhusu kuwa na mamilioni ya dola katika akaunti za benki nchini Switzerland.