Chimamanda Ngozi Adichie: Sura mpya ya vipodozi

Chimamanda Ngozi Adichie

Huenda mojawapo ya watu wanaotetea haki sawa za wanawake sio chaguo la kutarajiwa kuwa sura ya matangazo ya vipodozi kwa wanawake, lakini kampuni ya Boots imemfanya Chimamanda Ngozi Adichie kuwa sura ya bidhaa za urembo za No7.

Mwanatamthilia huyo wa Nigeria anafahamika katika majukwaa ya fasihi lakini aliongezeka umaarufu baada ya muibaji maarufu wa Marekani, Beyonce kutumia sehemu ya tungo yake ijulikanayo kama 'We Should all be Feminists' katika kibao chake cha mwaka 2014 'flawless'.

Sasa tungo zake zinatumiwa na kampuni ya Boots katika tangazo la biashara lililotolewa wiki hii: "kwa muda fulani niliacha kujipamba na nilivificha viatu vya mchuchumio. Na nikawa mtu asiye mimi. Lakini niliamka na nikaona kwa rangi kamili, kujiamini kikamilifu."

Kama mtu anayetetea haki saa za wanawake, anafahamu kwamba ni lazima aeleze uhusiano wake na vipodozi.

Katika hotuba aliotoa kwenye mazungumzo ya Ted Talk amesema kuwa na msimamo wa kutetea haki sawa za wanawake ni 'mzigo mkubwa'.

"Unawachukia wanaume, unachukia sidiria, unachukia utamaduni wa Kiafrika."

Badala yake anasema, alitaka kutambuliwa kama 'Muafrika mwenye raha anayetetea haki sawa za wanawake, asiyechukia wanaume, anayependa vipodozi na anayevaa viatu vya mchuchumio - kujifurahisha mwenyewe na sio kuvutia wanaume".