Mthembu:viongozi wa ANC wajiuzulu akiwemo rais Zuma

Jackson Mthembu Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Jackson Mthembu wa ANC

Mmoja wa viongozi wakubwa wa chama cha ANC cha Afrika ya kusini Jackson Mthembu amewataka viongozi wote wa chama hicho kujiuzulu akiwemo Rais Jacob Zuma na yeye mwenyewe.

Mthembu amesema kuwa wote wanatakiwa kuwajibika kwa sababu ya machafuko ndani ya chama.

ameeleza kuwa shutuma ya ubadhirifu inayomkabili waziri wa fedha Pravin Gordhan imechochewa na siasa.

Chama cha ANC kinamgawanyiko kwa sasa na kinapoteza wafuasi wake kwasababu ya kashfa za rushwa zinazomkabili Zuma na ukosefu wa ajira kwa watu. Mwezi wa nane chama hicho kilipata matokeo mabaya katika uchaguzi wa serikali za mitaa