Uturuki inajihami na kundi la IS karibu na Mji wa Mosul

Binali Yildirim Haki miliki ya picha Google
Image caption Binali YildirimWaziri mkuu wa Uturuki

Uturuki imesema vikosi vyake vilivyoko Iraq vimechukua hatua ya kujilinda dhidi ya kundi la kigaidi la dola la kiislamu karibu na mji wa Mosul huko Iraq, lakini serikali ya Iraq imekataa kuhusika kwake.

Waziri mkuu wa Uturuki Binali Yildirim amesema kuwa mizinga ya Uturuki imekuwa ikiwasaidia kundi la Kikurdi la Peshmerga kupambana na wanamgambo wa IS walio karibu na kambi ya Bashiqa mahali ambapo vikosi vya askari wa kituruki wamekuwa wakifunzwa mafunzo ya kijeshi.

Kundi la Peshmerga limesema kuwa limekamata mji wa Bashiqa, ulioko kilomita kumi na mbili kutoka mji wa Mosul. Na Uturuki imesisitiza kuwa lazima itashiriki kulinda mji wa Mosul.

Waziri mkuu wa Iraqi Haider al-Abadi amekanusha madai hayo, japokuwa Marekani imeshauri kufanyika kwa makubaliano.