Watu wanne wapoteza maisha Jamuhuri ya Afrika ya kati

Majeshi ya kulinda amani yaliingia nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati mwaka 2014 Haki miliki ya picha AFP
Image caption Majeshi ya kulinda amani yaliingia nchini Jamuhuri ya Afrika ya kati mwaka 2014

Watu wanne wameuawa wakati wa maandamano dhidi ya walinda amani wa Umoja wa mataifa nchini Jamuhuri ya Afrika ya kati.

Walinda amani walifyatua risasi wakati waandamanaji walipokuwa wakijaribu kuingia kwa nguvu kwenye jengo la makao makuu ya UN.Mwandishi wa BBC, aliyeshuhudia miili ikichukuliwa kwenye gari ya Polisi.

Umoja wa wataifa umesema haukutumia risasi za kweli na kusema wanajeshi wake walitumia gesi ya kutoa machozi tu.

Kundi la Raia wa Jamuhuri ya Afrika ya kati wanataka walinda amani wa UN kuondoka wakisema imeshindwa kuwalinda watu.

Walinda amani waliingia nchini humo baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kuanza mwaka 2013 ambapo aliyekuwa Rais wa kipindi hicho Francois Bozize ambaye aliondolewa na kundi la Seleka.

Umoja wa Mataifa umekuwa ukikumbwa na shutuma kadhaa kuwa vikosi vyake vimekuwa zikiwadhulumu watoto kingono.