EU na Canada zasema biashara huria haijafa

Brussels Haki miliki ya picha Reuters
Image caption kumekua na maandamano huko Brussels kupinga kutia saini kwa makubalino hayo

Canada na nchi za Umoja wa Ulaya zimesema kuwa biashara zake huria bado hazijafa, japokuwa maeneo matatu ya nchi ya ubelgiji yamegoma kutia saini.

Rais wa Baraza la Ulaya Donald Tusk, amesema kuwa bado kuna uwezekano wa kutiwa saini siku ya alhamis kama ilivyopagwa. Nae Waziri wa biashara wa Canada, Chrystia Freeland amesisitiza kuwa kwa sasa shauri hilo lipo kwenye mahakama ya umoja wa ulaya.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Chrystia Freeland Waziri wa biashara wa canada.

Freeland amesema bado kutakuwa na maswali magumu kuhusu sera ya biashara ya ulaya iwapo makubaliano hayo hayatawekwa saini.

Maeneo yote ya Ubelgiji yanalazimishwa kukubali mpango huo kabla ya serikali ya shirikisho kuungana na nchi nyingine za Umoja wa ulaya ili kutia saini. Japokuwa Maeneo matatu ya nchi ambapo lugha ya Kifaransa inazungumzwa na kuongozwa na wa socialist wadai kuongezwa kwa muda zaidi ili waweze kuusoma mkataba huo.

mamlaka za watu wanaozungumza Kiflemish zimesema kucheleweshwa huko ni sawa na kuiletea nchi hiyo matani.