Patel: Msaada lazima uwe na thamani ya kifedha

Priti Patel
Image caption Priti Patel akiwa nchini Kenya

Serikali ya Uingereza imesema kuwa imejiandaa kuondoa misaada kwenye miradi mikubwa ya mataifa mbalimbali isipokuwa itatoa huduma bora ya thamani ya kifedha.

Katibu mkuu wa miradi ya kimataifa Priti Patel, ameiambia BBC kuwa kiasi fulani cha bajeti ya misaada ya dola za Uingereza bilioni 15 lazima zitumike kwa ajili ya mpango wa kuanzisha biashara huria baada ya kuondoka umoja wa ulaya. Aliyasema hayo katika mahojiano na BBC nchini kenya.

Bi Patel amesema ikiwa watashindwa kufikia viwango walivyojiwekea, yupo tayari kupunguza kiasi hicho.

Asilimia 40 ya bajeti ya misaada ya uingereza imeelekezwa kwenye mashirika mbalimbali ya kimataifa ikiwemo benki ya dunia.