25 wafariki katika mapigano CAR

Walinda amani wa Umoja wa mataifa Jamhuri ya Afrika ya kati

Watu 25 wameuawa katika mapigano ya siku mbili katika Jamhuri ya Afrika ya kati , kikosi cha Umoja wa mataifa cha kulinda kimesema.

Watu 15 waliuawa Alhamisi katika mapigano kati ya wapiganaji waislamu wa lililokuwa kundi la Seleka na kundi la sungusunguwa kikristo anti-Balaka group, umesema.

Maafisa sita wa polisi na raia wanne wamefariki ika uvamizi siku ya Ijumaa

Kumeshuhudiwa ghasia katika Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa misingi ya kikabila na kidini tangu 2013.

Umoja wa mataifa unasema hali ya kuzuka upya kwa mapigano huko Jamhuri ya Afrika ya kati , ni ya kutia wasiwasi.

Vikosi vya umoja wa mataifa vilivyokuwa vinashika doria katika uwanja wa ndege mjini hapo pia vilishambuliwa.

Wito umetolewa kwa makundi hayo kinzani yasitishe uhasama mara moja.