Mlipuko wa bomu mjini Benghazi, Libya wauwa watu kadha

Ramani
Image caption Ramani

Bomu lililotegwa ndani ya gari, limelipuka na kuwauwa watu kadhaa katika mji wa Benghazi, nchini Libya.

Waliouwawa wanasemekana kuwa wanaharakati wa kisiasa wanaofahamika na wanaohusishwa na Jemedari mmoja anayeongoza kampeini ya miaka miwili, dhidi ya wanamgambo wa Islamic State.

Mohammed Bou-qa-i-qis ameuwawa kwa pamoja na watu wengine wawili, huku wengine zaidi ya kumi wakijeruhiwa vibaya.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mlipuko ndani ya gari

Amekuwa akiendesha kipindi cha kila siku cha Runinga huku akiahidi kuwaunga mkono wanaharakati wanaopinga kampeini za I-S, inayoongozwa na Jenerali Khalifa Hafter.

Usalama katikati mwa mji wa Benghazi umeimarika pakubwa, lakini mapigano viungani mwa mji huo, bado yanaendelea,

Maiti ya watu 10 ambao hawajulikani, ilipatikana siku ya Ijumaa, ikiwa inaonekana waliteswa hadi kufa.