Waziri mkuu wa Serbia ahamishiwa mahala salama

Aleksandar Vucic
Image caption Waziri mkuu Aleksandar Vucic

Maafisa wa polisi huko Serbia, wamemuondosha waziri mkuu wa nchi hiyo Aleksandar Vucic na familia yake, hadi maeneo salama, baada ya kupatikana kwa idadi kubwa ya silaha karibu na nyumbani kwake, kilomita kadhaa kutoka mji mkuu Belgrade.

Ugunduzi wa silaha hizo zikiwemo bunduki hatari za kurusha maroketi, magruedi yanayorushwa kwa mkono na makasha kadhaa ya risasi.

Waziri wa maswala ya ndani ya taifa hilo, Nebojsa Stefanovich, amesema kwamba silaha hizo zilipatikana karibu na njia panda mahali ambapo gari la waziri mkuu huwa inapunguza mwendo kabla ya kufika nyumbani kwake.

Image caption Waziri wa msawala ya ndani Nebojsa Stefanovic

Bwana Vuchich zamani alikuwa mwanamapinduzi na mwanaharakati mkubwa aliyekuwa akishinikiza kwa mataifa iliyokuwa muungano wa Usovieti kurejea pamoja na kuunda muungano huo, Lakini alibadilisha kauli yake na kuunga mkono ujumuishwaji wa mataifa hayo ndani ya muungano wa EU.

Polisi bado hawajamtia mbaroni mtu au kundi la watu wanaohusishwa na upatikanaji huo wa silaha.

Bado kungali na mamia kwa maelfu ya silaha haramu nchini Serbia, iliyoachwa wakati wa vita vya Yugoslavia vya miaka ya 1990.