Mke wa Trump amnadi mumewe hadharani

Amesema kuwa mume wake anaipenda Marekani na ameahidi kuifanya kuwa nchi yenye nguvu kwa mara nyingine
Image caption Amesema kuwa mume wake anaipenda Marekani na ameahidi kuifanya kuwa nchi yenye nguvu kwa mara nyingine

Mke wa mgombea urais Marekani kupitia chama cha Republican Melania Trump, ametoa hotuba ya kampeni isiyo ya kawaida kuhusu uchaguzi utakaofanyika Jumanne ijayo novemba 8.

Akizungumza katika jimbo la Pennsylvania, mke wa Trump alielezea majukumu yake kama mama na historia yake ya uhamiaji.

Amesema kuwa mume wake anaipenda Marekani na ameahidi kuifanya kuwa nchi yenye nguvu kwa mara nyingine.

Image caption Melania amesema tuhuma anazopewa mumewe juu ya unyanyasaji kwa wanawake ni uongo

Kwa upande mwengine Rais Obama amekuwa akiwashawishi wapigakura vijana katika jimbo la Florida kukiunga mkono chama cha Democtaic na Hillary Clinton.

Donald Trump aliwahi kuhutubia jimboni hapo, kabla ya kwenda North Carolina.

Bi Clinton pia ataenda kufanya kampeni jimboni hapo.