Mwanafunzi aliyempinga Mugabe akamatwa

Maandamano ya kumpinga rais Mugabe na sera zake yamekuwa mengi wakati nchi inakabiliwa na hali mbaya ya uchumi Haki miliki ya picha AP
Image caption Maandamano ya kumpinga rais Mugabe na sera zake yamekuwa mengi wakati nchi inakabiliwa na hali mbaya ya uchumi

Mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu amechukuliwa na watu wasiojulikana, baada ya kuonyesha bango lililokuwa na maandishi ya kumtaka rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ajiuzulu

Bwana Mugabe alikuwa akiongoza hafla ya kufuzu kwa wanafunzi wa chuo kiku cha Sayansi na Teknolojia cha Bulawayo kilicho kusini mwa Zimbabwe wakati kundi la wanafunzi lilifanya maamdamano.

Advance Musoke aliakuwa mmoja wa wanafunzi 14 waliokuwa wakifuzu walioiunu mabango kupinga ukosefu wa ajira. Haijulikani ikiwa Rais Mugabe aliona mabango hayo.

Makomborero Haruzivishe, ambaye ni kiongozi wa wanafunzi aliiambia bbc kuwa wanaume wasiojulikana walimchukua bwana Musoke huku wengine wakifanikiwa kutoroka.

Maandamano ya kumpinga rais Mugabe na sera zake yamekuwa mengi wakati nchi inakabiliwa na hali mbaya ya uchumi