Samsung yavamiwa kwa uchunguzi wa ufisadi wa kisiasa

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Park ameomba msamaha kwa uhusiano wa karibu na Bi Choi lakini anakabiliwa na miito ya kumtaka ajiuzulu.

Waendesha mashtaka nchini Korea kusini wamevamia ofisi za kampuni ya kielektoniki ya Samsung kama sehemu ya uchunguzi wa sakata ya kisiasa inayomuhusu rais Park Geun-hye.

Waendesha mashtaka wanachunguza madai kwamba Samsung ilimpatia pesa mtoto wa kike wa Choi Soon-sil, ambaye ni rafiki wa karibu wa rais.

Bi Choi anashutumiwa kutumia urafiki wao kuingilia kati siasa na utoaji wa zabuni za kibiashara.

Samsung imeithibitishia BBC kuwa uvamizi huo ulifanyika ikisema "hakuna maelezo zaidi ".

Rais Park ameomba msamaha kwa uhusiano wa karibu na Bi Choi lakini anakabiliwa na miito ya kumtaka ajiuzulu.

Haki miliki ya picha AFP/GETTY
Image caption Bi Choi Soon-sil alikamatwa tarehe 3 Novemba na kushtakiwa kwa makosa ya ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka.

Katika sakata ya hivi karibuni ambayo imeikumba Korea kusini katika wiki za hivi karibuni , waendesha mashtaka wanachunguza madai kwamba Samsung huenda ilitoa dola $3.1m kwa kampuni inayomilikiwa Bi Choi na mtoto wake wakike kwa ajili ya kulipia mafunzo ya mwanae wa kike ya kuendesha farasi mwanae nchini Ujerumani.

Waendesha mashtaka pia wanaripotiwa kujvamia ofisi ya korea kusini ya shirikisho la wamiliki wa farasi na pia ofisi za jumuiya ya masuala ya farasi ya Korea

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Park alisema anajuta kwa ''kuwa na imani ya kupita kiasi ''katika urafiki wake na bi Shoi

Bi Choi alikamatwa tarehe 3 Novemba na kushtakiwa kwa makosa ya ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka.

Kwa muda wa siku tatu zilizopita maelfu kwa maelfu ya raia wa Korea kusini wamekuwa wakiandamana katika mji mkuu , Seoul, kudai kujiuzulu kwa rais Park kutokana na sakata hiyo ya ufisadi.

Bi Park alikuwa rais wa kwanza mwanamke wakati alipochaguliwa katika uchaguzi uliokuwa na ushindani mkali mwezi Disemba 2012.