Mwanamfalme Harry alaani matusi ya wanahabari kwa mpenziwe

Mwanamfalme Harry na Bi Markle Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Taarifa ya taasisi ya habari ya Mwanamfalme ilisema: wapenzi hao "waliingia katika mahusiano yao miezi michache " na kwamba "haikuwa haki " kwa Bi Markle kutendewa dhihaka.

Mwanamfalme Harry amethibitisha kuwa muigizaji wa Marekani Meghan Markle ni mpenzi wake, katika kauli aliyoitoa kutoka kwenye kasri ya Kensington Palace akishambulia vyombo vya habari kwa kumuweka mpenziwe katika "wimbi la la matusi na mateso".

Taarifa hiyo ilisema wapenzi hao "waliingia katika mahusiano yao miezi michache " na kwamba "haikuwa haki " kwamba Bi Markle alipaswa kutendewa dhihaka.

Ilisema ni nadra kwa mwanamfalme kuchukua hatua rasmi "juu ya taarifa zisizo za kuaminika". " Lakini wiki iliyopita aliona mashambulio dhidi ya mpenziwe yamevuka kikomo ," iliongeza kuelezea taarifa hiyo.

Mnamo siku za hivi karibuni magazeti kadhaa yalichapisha kwenye kurasa zake za mbele taarifa kuhusu muigizaji mwenye umri wa miaka miaka 35- Rachel Zane, anayefahamika zaidi kwa mchezo wa maigizo wa televisheni.

Taarifa iliyotolewa na idara ya mawasiliano ya mwanamfalme Harry ilisema : "mpenzi wake wa kike, Meghan Markle, aliwekwa katika hali ya matusi na kunyanyaswa''.

"Baadhi ya haya yametangazwa sana kwa umma - kuwekwa katika kurasa za mbele za gazeti la taifa; maandishi ya kauli za ubaguzi ;na kauli za ubaguzi wa kijinsia pamoja na za ubaguzi wa rangi zilizotumwa kwenye mitandao ya habari ya kijamii na kauli za mtandaoni.

"baadhi yalifichwa kwa umma Some -vita vya usiku vya kisheria vya kujzujwia taarifa za matusi ziondolewe kwenye magazeti; mama yake kuhangaika na picha zake za zamani kwa waandishi waliotaka kufika kwake ; jaribio la maripota na wapiga picha kuingia kwake kinyume cha sheria nyumbani kwake na simu kutoka kwa polisi zilizofuatia ; hongo za mara kwa mara zilizotolewa na magazeti kwa mpenzi wake wa zamani; kusakwa kwa karibu kila rafiki yake na yeyote anayempenda maishani mwake''

Haki miliki ya picha PA
Image caption Miongoni mwa uigizaji wa Meghan Markle ni pamoja na filamu ya Horrible Bosses ya mwaka 2011

Mwanamfalme huyo mwenye umri wa karibu miaka 32- amekuwa na uhusiano mgumu na vyombo vya habari, ambapo katika ukuaji wake alielewa fika athari ya kuingiliwa na vyombo vya habari katika maisha ya marehemu mama yake, Diana, binti mfalme wa Wales.

Alipokuwa na umri wa miaka 20, alijipata katika mtego wa wapiga picha wa mapaparazzi nje ya jiji la London katika ukumbi wa burudani za usiku.

Mwaka 2012, picha zake za utupu akiwa katika chumba cha hoteli ya Las Vegas zilitumwa kwenye mtandao na kwenye kurasa za kwanza za magazeti suala lililoifanya taasisi yake ya habari itume malalamiko kwa tume ya taifa ya habari inayopokea malalamiko.