Timu ya Azam Fc yasaka vipaji

Tz Haki miliki ya picha Azam Fc
Image caption Vijana wakionesha vipaji vyao

Vijana saba wenye umri chini ya miaka 17, wamepenya kwenye majaribio ya wazi ya mwisho katika mkoa wa Dar es Salaam, yaliyoendeshwa na Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC leo Jumamosi.

Huo ni mwendelezo wa mpango wa mabingwa hao wa kutengeneza timu bora ya vijana wa umri huo kwa ajili ya kuwatumia kwa miaka ijayo na wengine kunufaika nao kwa kuwauza.Katika majaribio hayo walijitokeza vijana 433 wenye umri tofauti kuanzia chini ya umri wa miaka 10, 12, 14 na 17, ambapo kuchaguliwa saba pekee na wengine 33 kuorodheshwa.

Mpaka sasa mpango huo umeshahusisha maeneo matano tofauti nchini katika mkoa wa Dar es Salaam, Tanga, Morogoro, Dodoma na Visiwani Zanzibar, ambako kote kumefanya idadi ya vijana waliofanyiwa usaili kufikia 2,593, kati ya hao 50 pekee ndio waliochaguliwa kushiriki fainali ya mwisho itakayofanyika Uwanja wa Azam Complex mwezi ujao.Mbali na vijana hao 50, wengine 96 wameorodheshwa na kuhifadhiwa kama akiba ya baadaye.