Iraq yaukomboa mji wa Nimrud

IRAQ Haki miliki ya picha AFP
Image caption Picha zenye michoro zikibomolewa

Vikosi vya serikali vya Iraq vinasema wameikomboa Nimrud eneo la mji wa kale wa kusini mwa Mosul ambao ulikuwa ukidhibitiwa na wapiganaji wa kundi la Islamic State miaka miwili iliyopita.

Mji huo wa kale ambao mwanzoni ulikuwa mji mkuu wa dola ya Waashuri , ulikuwa umeharibiwa vibaya na wanamgambo hao wa dola ya kiislam I-S mwaka uliopita, kitendo hicho kilishutumiwa wazi wazi na Umoja wa Mataifa kuwa ni uhalifu wa kivita.

Jeshi la Iraq limetoa tamko kuwa limeurudisha tena mji mwengine mpya kwenye himaya yake yake karibu na mji huo wa kale wa Nimrud, pamoja na kijiji kingine karibu na mji huo.

Islamic State walikuwa wakiuchukia mji huo wa kale wa Nimrud kwa uujibu wa imani yao ambao awali ulisheheni sanamu za viumbe vya kufikirika kuwa havichangamani na dini yao ya kiislamu.