Dondoo za michezo mwishoni mwa wiki

Tanzania Haki miliki ya picha Google
Image caption Mbwana Samatta

Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, jana ilikuwa na mechi ya Kirafiki na Zimbabwe.Pamoja na Safu ya ushambuliaji ya Tanzania kuongozwa na Mbwana Ally Samatta lakini watanzania waliishia kuambulia kichapo cha mabao matatu patupu.

Katika kufuzu kucheza Kombe la Dunia litakalofanyika mwaka 2018 nchini Urusi, Uganda iko vizuri katika nafasi ya pili nyuma ya Misri katika kundi E baada ya kuwabamiza Congo Brazaville bao moja kwa sifuri.

Jana Jumapili majirani wa Congo Brazaville, hapa nawazungumzia DRC wao wakawabamiza Guinea nyumbani kwao bao 2-1 na hivyo kuongoza kundi A.Na kule mjini Alexandria, Misri ikawabamiza Ghana bao 2-0 .

Majina ya wachezaji watano wanaowania Tuzo ya BBC ya Mwanasoka Bora wa Afrika kwa Mwaka 2016 yameshatangazwa.Wachezaji hao ni Pierre-Emerick Aubameyang, Andre Ayew, Riyad Mahrez, Sadio Mane and Yaya Toure.

Hadi tarehe 28 ya mwezi huu endelea kupiga kura kupitia bbc.com/africanfootball, mimi na wenzangu tutaendelea kukupa habari kuhusu shindano hili kwa kadri tuwezavyo mpaka pale tarehe 12 Desemba, mshindi wa tuzo hiyo atakapotangazwa.

Na hatimaye mashindano ya kimataifa ya mbio za baiskeli Tour of Rwanda yanatimua vumbi nchini Rwanda ambapo leo washindani 75 wanaelekea mkoa wa mashariki.