Obama asisitiza ushirikiano kimataifa

Marekani na Urusi wateta
Image caption Rasi wa Urusi Vladmir Putin na Rais mteule wa Marekani Donald Trump

Ikulu ya Urusi imesema kwamba rais Vladimir Putin amezungumza kwa njia ya simu na rais mteule wa Marekani Donald Trump, pamoja na mambo mengine amempongeza kwa ushindi aliopata,Putin amesema kwamba anaahidi kufanya kazi pamoja na rais huyo wa Marekani Donald huku akitilia mkazo suala la uhusiano wa nchi hizo mbili.

Wakati wa harakati zake za kampeni, Trump aliendelea kurudia rudia kumpongeza rais huyo wa Urusi, akimuelezea kama mtu mwenye upeo mkubwa ukimlinganisha na rais anayeondoka madarakani Barack Obama.

Wakati huo huo.

RAIS Barack Obama amewahakikishia washirika wa Marekani kwamba Donald Trump ataendeleza heshima na ushirikiano wa kimataifa baina ya nchi yake nao wakati yeye atakapokabidhi urais mwezi Januari.

Obama ameyasema hayo wakati alipokuwa na mkutano mkubwa na waandishi habari .

Rais Obama amesema kwamba Donald Trump ameonesha nia ya kutaka kudumisha uhusiano baina ya Marekani na shirika la nuklia duniani NATO.

Obama amesema kwamba Marekani lazima iendelee kuwa nguzo ya nguvu na nguzo ya matumaini kwa watu duniani kote.

Na kuongeza kusema kwamba uhusiano baina ya nchi na nchi unakwenda mbali zaidi ya nafasi ya urais na wanadiplomasia,majeshi na kwamba wakuu wenye hekima na busara wataendelea kuonesha ushirikiano na wenzao wanaoshughulikia masuala ya kigeni.

Obama alikuwa akizungumza kuelekea mwishoni mwa safari zake za mataifa ya kigeni akiwa mwishoni mwa madaraka yake ya urais.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii