Scott Pruitt kuwa Waziri wa mazingira Marekani

Rais amteule wa Marekani Trump amteua Scott Pruitt
Image caption Rais mteule wa Marekani Trump amteua Scott Pruitt

Rais mteule wa Marekani Donald Trump amemteua mwanasheria mkuu wa jimbo la Oklahoma Scott Pruitt kuwa Waziri wa mazingira.

Pruitt anaonekana kuwa mshirika wa sekta ya mafuta ambaye amekuwa akipingana na sera ya Rais Baraka Obama juu ya mabadiliko ya tabia nchi.

Katika kampeni za uchaguzi wa rais Trump amefafanua mpango wa nishati safi kama vita dhidi ya makaa ya mawe na kusema kuwa Marekani inapaswa kujitoa katika mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabia nchi na kusema kuwa ongezeko la joto duniani ni kama utapeli au uzushi.