Miss.Tanzania apambana na ukeketaji nchini Tanzania
Huwezi kusikiliza tena

Miss Tanzania apambana na ukeketaji nchini Tanzania

Inakadiriwa kuwa wasichana wapatao milioni 200 wamefanyiwa ukeketaji mpaka sasa ulimwenguni kote.

'Dondosha wembe' ni moja ya kampeni inayoendelea nchini Tanzania ikiwa na lengo la kutokomeza mila hiyo potofu.

Lakini je, kampeni hiyo inafanyikaje? Mwandishi wa BBC, Esther Namuhisa alizungumza na Miss Tanzania 2016/2017 Diana Edward, mwanzilishi wa kampeni hiyo.