Michael Flynn kuchunguzwa?

Marekani
Image caption Michael Flynn, mshauri wa masuala ya usalama nchini Marekani

Kiongozi wa chama cha Democratic Nancy Pelosi amemtaka raisi wa Marekani Donald Trump kumfukuza kazi mshauri wake wa masula ya usalama wa taifa hilo, Michael Flynn, hatua hii inakuja baada ya kugundulika kuwa Flynn alikuwa na mazungumzo kuhusiana na vikwazo dhidi ya Marekani na balozi wa Urusi muda mfupi kabla ya Raisi Trump hajachukua hatamu za madaraka.

Bi Pelosi amesema kwamba generali Flynn anaweza kuwa si mtu wa kumuamini na anaweza kuweka maslahi ya Marekani nyuma na kuweka maanani jjua ya Urusi, na kwamba baadaye anaweza kuudanganya umma wa wamarekani juu ya mawasiliano yake.

Imefahamika pia kuhusiana na mawasiliano yake na shirika la upelelezi la Marekani FBI na uchunguzi wake juu ya uhusiano wa raisi Trump na raisi wa Urusi , Vladimir Putin.

Ikulu ya Marekani imetoa maelezo kuwa Rais Trump anatathmini mazingira ya mshauri wake huyo General Flynn .