McMaster awa mteule mpya wa Rais Trump

Luten Generali Herbert Raymond mshauri mpya wa masuala ya usalama Marekani
Maelezo ya picha,

Luten Generali Herbert Raymond mshauri mpya wa masuala ya usalama Marekani

Rais Donald Trump amemteua Luten Generali Herbert Raymond McMaster kuwa mshauri mpya wa usalama.

Uteuzi huo mpya ni kufuatia kufutwa kazi kwa Luteni Generali Lt Gen Michael Flynn ambaye alihudumu katika cheo hicho kwa wiki tatu tu.

Mteule wa sasa wa Rais Trump yaani Luteni Generali McMaster alifanya kazi nchini Iraq na Afghanistan alikokuwa katika kitengo cha kukabiliana na rushwa.

Rais Trump amempongeza McMaster kukubaliana na uteuzi huo na kumuelezea kuwa ni mtu mwenye uzoefu mkubwa na anayeheshimika na kila mmoja.

Katika kitabu chake McMaster aliwahi kulalamikia uamuzi wa majeshi ya Marekani kuhusika na vita vya Vietnam.

Ni msomi wa masuala ya historia ya Marekani kutoka chuo kikuu cha North Carolina.