Unicef yatangaza baa la njaa kwa nchi nne

Watoto milion moja na nusu kukumbwa na baa la njaa
Maelezo ya picha,

Watoto milion moja na nusu kukumbwa na baa la njaa

Shirika la kimataifa la kuhudumia watoto duniani Unicef limesema kuwa watoto milioni moja na nusu wapo katika hali mbaya kutokana na njaa katika nchi nne duniani.

Nchi hizo ambazo UN imezitangaza kuwa zinakabiliwa na njaa mapema siku ya jumatatu ni South Kusini, Yemen, Nigeria na Somalia.

Kumekuwa na ongezeko la tishio la njaa piaKaskazini mwa Nigeria,ambako mamilioni ya watu wameyakimbia makazi yao kutokana na wapiganaji wa Boko Haram.

Nchini Yemen pia hali ni mbaya kutokana na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe hali iliyosababisha idadi kubwa ya maisha ya watoto kuwa mashakani kutokana na uhaba wa chakula.

Nchini robo ya watu walikufa katika janga la njaa nchini humo la mwaka 2011 ambapo dalili zinaonyesha kuwepo uwezekano wa kuzuka baa la njaa kama hilo lililowahi kutokea miaka ya nyuma ambapo walishuhudia kushuka kwa bei ya mifugo na kupanda kwa bei ya chakula.