Marufuku matumizi ya anasa:Kashmir

Vyakula na matumizi ya anasa marufu sasa Kashmir
Maelezo ya picha,

Vyakula na matumizi ya anasa marufu sasa Kashmir

Serikali ya Jimbo la Kashmir nchini India imeweka zuio dhidi ya gharama za anasa.

Wazazi wa bibi harusi watapigwa marufuku kualika zaidi ya wageni mia tano, au mia nne ikiwa mtoto wa kiume atakuwa anaoa.

Idadi ya aina ya vyakula kwenye sherehe itakuwa saba, huku mziki wa sauti ya juu na fataki vitapigwa marufuku.

Serikali ya kashmir imesema imechukua hatua hiyo baada ya kuwepo kwa malalamiko ya watu kuhusu matumizi makubwa wakati wa sherehe na kelele zinazowakera wengine.

Amri hizo zitaanza kufanya kazi mwezi Aprili