Rais Trump kuongeza vigezo, kukabiliana na wahamiaji

Rais Donald Trump
Image caption Rais Donald Trump

Wizara ya usalama wa ndani ya nchi, huko Marekani, ina mipango ya kuwaajiri maelfu ya maafisa wa ziada.

Watakaohusika kutimiliza hatua kali zilizowekwa na utawala wa Donald Trump, kukabiliana na wahamiaji haramu. Maelekezo hayo yametolewa baada ya utawala wa Trump kusema kuwa, wahamiaji wasio na stakabadhi maalum ya kuishi Marekani na walio na rekodi ya uhalifu, wanahatarisha maisha ya Waamerika au wale ambao wamewahi hujumu mfumo wowote nchini Marekani.