Mexico yaponda sheria za uhamiaji za Marekani

Waziri wa mambo ya kigeni wa Mexico Luis Videgaray
Maelezo ya picha,

Waziri wa mambo ya kigeni wa Mexico Luis Videgaray

Mexico imeilaumu Marekani kuhusiana na sheria zake za uhamiaji katika kuwaondoa wahamiaji wasio na vibali.

Kuhusiana na mpango wa Rais Trump uliotangazwa siku ya jumanne ni kwamba wale wote waishio kinyume cha sheria watalengwa na hatua ya kuondolewa nchini humo.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Mexico Luis Videgaray amesema taifa lake halitakubaliana na maamuzi hayo yanayotolewa na taifa moja dhidi yam engine.

Hatua hii inakuja wakati viongozi wa juu wa wawili wa Marekani wakiwa na mpango wa kuitembelea Mexico.

Ikulu ya Marekani kupitia mkuu wake Rex Tillerson na bwana wanatarajiwa kuwa na mazungumzo kuhusiana na namna ya utekelezaji wa vigezo hivyo vipya vya uhamiaji.

Hata hivyo haijafahamika mara moja kama Marekani ina mamlaka kuilazimisha Mexico kupokea raia wa kigeni.

Lakini Waziri wa mambo ya kigeni wa Mexico Videgaray amesema jana kuwa hawatakubaliana na sera hiyo na pia haina maslahi yoyote kwa taifa la Mexico.