Kimbunga Doris chaua Uingereza

Makazi ya Watu yameachwa bila huduma ya umeme

Chanzo cha picha, PA

Maelezo ya picha,

Makazi ya Watu yameachwa bila huduma ya umeme

Mwanamke mmoja amepoteza maisha na watu wengine wawili wamejeruhiwa vibaya, baada ya kimbunga Doris kupiga mji wa Wolverhampton nchini Uingereza kwa kasi ya kilomita 94 kwa saa.

Imeelezwa kuwa mwanamke huyo alipata majeraha kichwani baada ya vipande vya mabaki ya vitu kuanguka katika mtaa mjini humo.

Upepo huo mkali umesababisha safari za ndege kusitishwa huku pia huduma za usafiri wa barabara na reli kusimamishwa.

Maelfu ya makazi na biashara zipatazo 1,500 kaskazini mwa Ireland zimeachwa bila ya huduma za umeme, huku milingoti na nyaya ya umeme zikiangukiwa na miti.

Taarifa kutoka kwa shirika la kawi nchini Uingereza imesema kuwa, karibu watu 12, 030 hawana nguvu ya umeme.