Mourinho: Wachezaji wenye ubinafsi walimsaliti Ranieri

Mourinho asema wachezaji wa Leicester walimasliti Ranieri
Maelezo ya picha,

Mourinho asema wachezaji wa Leicester walimasliti Ranieri

Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho amewashutumu wachezaji wa Leicester kwa kuwa na ubinafsi wa kumsaliti aliyekuwa mkufunzi wao Claudio Ranieri.

Mkufunzi huyo alivaa kofia yenye nembo za CR akimuunga mkono Claudio Ranieri kabla ya kuwashutumu wachezaji hao ambao wengi wao walisaini kandarasi mpya baada ya kushindi taji la ligi.

Muorinho alifutwa kazi katika mandhari kama hayo msimu uliopita kufuatia mgomo wa wachezaji lakini akasema kuwa kisa alichofanyiwa kilikuwa kidogo sana ikilinganisha na vile Ranieri alivyofanyiwa.

''Nadhani msimu huu ulianza na ubinafsi mwingi wachezaji wakitaka kupewa mikataba mipya'' .

''Watu wakifikiria fedha zaidi wengine wakiamua kuondoka bila kujali ni nani aliyewafanya kufikia walivyo'' alisema Mourinho.