Mchoraji mahiri asiyeona nchini Uganda
Huwezi kusikiliza tena

Mchoraji mahiri asiyeona nchini Uganda

Msanii Ritah Kivumbi anapenda sana tasnia ya Sanaa ya uchoraji ijapokuwa ni mtu asiyeona. Alipoteza uwezo wa kuona alipokuwa mtu mzima na sasa hawezi kuajiriwa tena. Pendo lake la sanaa ya uchoraji liliongezeka ingawa ana papasapapasa tu huku akifanya michoro ambayo anafiikiria. Mwandishi wetu Siraj Kalyango alifika katika studio yake na kuona jinsi anavyochora picha hizo.