Trump amfuta kazi muendesha mashtaka wa Manhattan

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Preet Bharara awali aliombwa na Trump kutojiuzulu

Nchini Marekani, muendesha mashtaka wa jimbo la Manhattan, amefutwa kazi na Rais Donald Trump.

Preet Bharara, ni mmojawepo wa waendesha mashtaka 46 walioteuliwa na Rais Baraack Obama, na ambao walishauriwa na Naibu Mwanasheria Mkuu kujiuzulu.

Bwana Bharara, alikataa kujiuzulu, baada ya kuambiwa binafsi na Trump, kusalia kwenye cheo chake muda mfupi baada ya uchaguzi mkuu wa Urais mwezi Novemba.

Kupitia mawasiliano ya mtandao wa kijamii wa Twitter, Bwana Bharara, ameelezea kinaga ubaga kuwa, hajajizulu bali amefutwa kazi.

Amezungumzia swala la kuwa muendesha mashtaka mkuu huko Manhattan, kama hatua kubwa kwa taaluma.