Uchunguzi wa ugaidi, kuanzishwa Ufaransa

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Polisi wanasaka nyumba ya Belgacem, kaskazini mwa Paris kubaini iwapo ana uhusiano na wapiganaji wa kigaidi

Taarifa zaidi zinazidi kuchipuka, kuhusiana na mtu ambaye alipigwa risasi na kuuwauwa alipojaribu kumpokonya bunduki askari, kwenye wa ndege wa Orly, karibu na mji mkuu wa Ufaransa, Paris.

Muendesha mashtaka, Francois Molins, amesema kuwa mshukiwa huyo mwenye umri wa miaka 39, aliyetajwa kuwa Zied ben Belgacem, alikuwa amewaambia askari hao, kuweka chini silaha zao, huku akisema kuwa yuko tayari "kufa kwa ajili ya Allah".

Kitabu cha Quran kilipatikana mwilini mwake.

Bwana Molins, amesema pia kuwa, mtu huyo alipokea mafunzo yenye itikadi kali akiwa gerezani, alikofungwa kwa makosa ya kupatikana na dawa za kulevya, miaka sita iliyopita.

Operesheni ya kuwasaka magaidi inaendelea nchini Ufaransa.