Federer atwaa taji kwa kumchapa Wawrinka

Roger Federer Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Roger Federer

Mcheza Tenesi Roger Federer ametwaa taji la wazi la BNP Paribas baada ya kumchapa Stan Wawrinka kwa 6-4 na 7-5.

Wawrinka anayeshika nafasi ya tatu kwa ubora alianza kwa kuongoza kwa 2-0 kabla ya Federer kurudisha na kumfunga mfululizo mpinzani wake huyo.

Mchezo huu ulikuwa ni wa 23 kwa nyota hawa wa tenesi kuchuana.

Elena Vesnina nae ametwaa taji la michuano hiyo kwa upande wa wanawake kwa mkumshinda Svetlana Kuznetsova 6-7 (6-8) 7-5 6-4.