Brazil yaichapa Uruguay

Brazil Haki miliki ya picha PA
Image caption Mfungaji wa mabao matatu ya Brazil Paulinho

Timu ya taifa ya Brazil wameibuka na ushindi ugenini kwa kuichapa Uruguay kwa mabao 4-1. katika mchezo ya kuwania kufuzu kwa kombe la dunia la mwaka 2018.

kiungo Paulinho akifunga hatrick na Neymer akifunga bao moja, huku bao pekee la Uruguay likifungwa na mshambuliaji Edson Cavan kwa mkwaju wa penati.

Katika michezo Colombia waliibuka na ushinda kwa bao 1 - 0 dhidi ya Bolivia goli la Colombi, likiwekwa kambani na mshambuliaji mahiri wa timu hiyo James Rodrigues.

Argentina wakapata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Chile. Bao pekee la Argentina likifungwa na Lionel Messi kwa mkwaju wa penati.

Paraguay wakawachapa Ecuador 2-1. Nao Venezuela wakatoshana nguvu na Peru kwa sare ya 2 - 2.