Ukosefu wa vibanzi katika ratiba ya mlo unawanyima raha wastaafu Ufaransa

VIBANZI AU CHIPS Haki miliki ya picha YOUTUBE

Wazee wanaoishi katika makaazi ya kustaafu nchini Ufaransa wameghadhabishwa sana kwa kutoandaliwa vibanzi katika mlo wao kiasi cha kulalamika kwa meya wa mji.

Wakaazi wa nyumba ya wazee ya Hubiliac huko Saint-Marcel, wametamani sana vibanzi ambavyo hawajaandaliwa tangu mwaka 2015, wakati mashine ya kuvikaanga ilipoharibika.

Huku ukame wa vibanzi hivyo ukiwa hautarajiwi kumalizika hivi karibuni wameamua kuwasilisha malalamiko rasmi kwa wasimamizi wa makaazi hayo na utawala wa mji unaohusika katika kuendeshwa kwa makaazi hayo, gazeti la Journal de Saone-et-Loire linaripoti.

"Watu wengi walijisajili kupata mlo siku ambapo kumepikwa vibanzi, ni kweli", anakiri msimaizi wa makaazi hayo Elisabeth Moreau, lakini ameshangazwa na jinisi suala hilo limefanywa kuwa kubwa.

Meya Raymond Burdin amewaambia wazee hao kwamba watalazimika kuwa na subira. "Inabidi tukagua mashine zote zisizofanya kazi na kununu mashini ya kukaanga vibanzi ni ghali kiasi ya euro 4000, kwahiyo inabidi musubiri mpaka kazi itakapokamilika" - Analaumu utepetevu wa utawala uliokuwepo wa mji.

Amewahakikishia kuwa kufikia mwaka ujao tataizo litatatuliwa, lakini "kwa sasa, vibanzi havipo kwenye ratiba ya chakula".