Wasichana na vita dhidi ya dawa za kulevya
Huwezi kusikiliza tena

Wasichana na vita dhidi ya dawa za kulevya Tanzania

Ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusiana na Dawa za Kulevya na Uhalifu ya mwaka 2016 inaonesha kuwa wanawake ambao wanatumia dawa za kulevya na ambao wameambukizwa virusi vya ukimwi wamekuwa wakinyanyapaliwa zaidi na kutokuwa na usalama kushinda wenzao wa kiume. Wamekuwa pia ni waathiriwa zaidi wa manyanyaso.

Aidha nchini Tanzania wasichana wanaotumia dawa za kulevya wengi wamejikuta wameingia kutokana na vishawishi vya marafiki zao wa kiume, huku wengine wakilazimishwa na marafiki zao hao kujiuza ili kupata fedha kununua dawa hizo.

Halima Nyanza amezungumza na baadhi ya wasichana walio katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya na baadhi kuguswa na yote hayo.