Tangazo la kupotosha la mafuta ya 'NIVEA' lazua hisia

Mafuta ya mwilini ya Nivea Haki miliki ya picha NIVEA Facebook
Image caption Mafuta ya mwilini ya Nivea

Mafuta ya mwilini kutoka Ujerumani NIVEA yameomba radhi na kuondoa tangazo lililodaiwa kuwa la kibaguzi.

Tangazo hilo lilisema kuwa ''weupe ni usafi'' likiwa na picha ya mwanamke mweupe.

Lilichapishwa katika mtandao wa facebook wa kampuni hiyo likiwa na lengo la kuwavutia wateja wake huko mashariki ya kati.

Nivea imekubali kwamba tangazo hilo linapotosha.

Wengi katika mitandao ya kijamii walilalama kuwa chapisho hilo ni la kibaguzi huku waliounga mkono tangazo hilo pia wakilisambaza.

Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Maoni yaliotolewa na wateja wa Nivea

Tangazo hilo katika facebook ya Nivea ambalo tayari limeondolewa lilichapishwa pamoja na maandishi: Keep it Clean, Keep it Bright{ jiweke msafi ung'are, Usikubali chochote kukuharibia}.

Tangazo hilo liliwalenga wateja wake huko mashariki ya kati ijapokuwa kampuni hiyo ina wafuasi milioni 19 duniani katika ukurasa wake.

Ikiomba radhi Nivea iliandika hivi: Kumekuwa na malalamishi kuhusu ubaguzi wa rangi kufuatia chapisho la Nivea kwa watu weusi na weupe katika ukurasa wa Nivea wa facebook.

Tunamuomba radhi mtu yeyote ambaye ameathiriwa na chapisho hili. Baada ya kubaini kwamba tangazo hilo linapotosha tuliliondoa kwa haraka.Tofauti za rangi na fursa sawa ni maadili ya NIVEA.