Wajumbe wa kamati maalum ya madini Tanzania wateuliwa

Image caption Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli

Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, leo Jumatatu ameteua kamati maalum ya pili, itakayofanya uchunguzi wa madini yaliyomo kwenye mchanga, ndani ya makasha yaliyoko katika maeneo mbalimbali nchini humo.

Kamati hiyo inajumuisha wanauchumi pamoja na wanasheria wa kamati ya kwanza iliyoundwa na wataalamu wa masuala ya Jiolojia, Kemikali na uchambuzi wa kisayansi.

Image caption Orodha ya wajumbe hao yenye majina manane

Hayo ni kwa mjibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.

Wajumbe hao wanane walioko kwenye orodha hiyo, wataapishwa kesho Jumanne asubuhi katika Ikulu ya Rais Jijini Dar es Salaam.