Syria kikaangoni, Baraza la Usalama, kupigiwa kura leo

Shambulio lililoipiga Syria

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Shambulio lililoipiga Syria

Wanadiplomasia wa Marekani wamesema wanatarajia Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa kupiga kura leo juu ya azimio la kwanza linalotaka Syria kushirikiana na Wachunguzi juu ya shambulio la wiki iliyopita, linalodhaniwa kuwa ni la kemikali.

Shambulio hilo lililofanywa katika mji unaoshikiliwa na waasi wa Khan Sheikhooun, liliua takriban watu tisini.

Wanadiplomasia hao wanasema wanaamini kwamba Urusi itazuia azimio hilo, ambalko limeandaliwa na Marekani, Uingereza na Ufaransa.

Iwapo Moscow itatumia kura yake ya VETO, itakuwa ni mara ya nane, ikizuia mshirika wake Syria kuchukuliwa hatua.