Ahmadinejad kuwania urais licha ya kuonywa na Khamenei

Bw Ahmadinejad amewaambia waandishi habari kuwa hilo lilikuwa "tu ushauri"

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Bw Ahmadinejad amewaambia waandishi habari kuwa hilo lilikuwa "tu ushauri"

Rais wa zamani wa Iran Mahmoud Ahmadinejad, amejiandikisha kuwa mgombea kiti cha urais kwenye uchaguzi mkuu nchini humo, licha ya kuonywa na mahakama kuu ya nchi hiyo kutogombea.

Bw Ahmadinejad, mwenye msimamo mkali na ambaye alihudumu kama Rais kwa mihula miwili kati ya mwaka 2005 na 2013, aliwasilisha makaratasi yake katika makao makuu ya Wizara ya ndani ya nchi hiyo ya kuwania kiti cha urais utakaofanyika Mei 19 mwaka huu.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Wagombea kiti cha urais watapigwa msasa na baraza lenye nguvu la Guardian

Mwaka jana, Ayatollah Ali Khamenei alimuonya kuwa, hatua kama hiyo "si katika maslahi yake na ya taifa".

Lakini Bw Ahmadinejad amewaambia wandishi habari kuwa hilo lilikuwa "tu ushauri".

Mwaandishi mmoja wa shirika la habari la Associated Press, aliyeshuhudia Bw Ahmadinejad akijiandikisha siku ya Jumanne, amesema kwamba maafisa wa uchaguzi "walishangaa" walipomuona akiwasilisha makaratasi hayo.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Bw Ahmadinejad, anasema anamuunga tu mkono mgombea Hamid Baqai

Rais Hassan Rouhani, mwanasiasa mwenye msimamo wa kadri na ambaye alihusika katika mjadala wa muafaka wa nuklea na viongozi wa mataifa yenye nguvu duniani mwaka 2015, bado hajawasilisha makaratasi yake, lakini anatazamiwa na wengi kugombea tena kiti cha urais kwa muhula wa pili.

Zaidi ya watu 120, wakiwemo wanawake 6, wamewasilisha majina yao katika siku ya kwanza ya kuajiandikisha hapo Jumatatu, hii ni kwa mjibu wa vyombo vya habari nchini humo.