Sylvester Stallone aishtaki Warner Bros

Sylvester Stallone

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Stallone aliigiza katika filamu ya Demolition Man pamoja na Wesley Snipes.

Sylvester Stallone anaishitaki studio ya filamu ya Warner Bros kwa kukosa kumpa kiwango cha pesa walichokubaliana kama faida, kutoka filamu ya mwaka 1993 ya Demolition Man.

Stallone anasema filamu hiyo ilitengeneza dola milioni 125 kwenye box office na kulingana na mkataba wake na studio hiyo, anastahili kupewa asilimia 15 ya pesa hizo.

Stallone anasema "studio za Motion Picture wanajulikana kuwa walafi" na warner Bros "walizuia fedha zangu" kwa miaka "bila ya sababu yoyote ile."

Warner Bros bado haijasema lolote kuhusu hatua hii ya kisheria.

Makaratasi ya kisheria ya Stallone yanaonyesha kuwa wawakilishi wake walijadili swala hilo na Warner Bros mwaka wa 2014 lakini waliarifiwa kuwa kampuni hiyo ya filamu haiwezi kumlipa Stallone chochote kwa sababu filamu ya Demolition Man ilipoteza dola milioni 66.9.

Stallone alihoji uamuzi huu na mwezi Aprili mwaka 2015 kampuni hiyo ilimtumia Stallone hundi ya dola milioni 2.8.

Kesi hii imefikishwa mbele ya mahakama ya Los Angeles na Stallone anataka ukaguzi wa pesa zote kutoka kwa filamu hiyo ufanywe.

Stallone aliigiza katika filamu ya Demolition Man pamoja na Wesley Snipes.