Tahadhari ya mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu Somalia

Vifo 533 kutokana na cholera au kuhara vimerekodiwa kufikia sasa
Maelezo ya picha,

Vifo 533 kutokana na cholera au kuhara vimerekodiwa kufikia sasa

Shirika la afya Duniani WHO, imetoa tahadhari ya kuokea kwa janga la ugonjwa wa kipindupindu na kuhara nchini Somalia katika miezi michache ijayo, haya ni kwa mjibu wa taarifa zilizochapishwa na shirika la habari la Reuters.

Taarifa hiyo inaongeza kuwa, kufikia sasa zaidi ya watu 25,000 wameambukizwa, na huenda idadi hiyo ikaongezeka.

Maelezo ya picha,

Ramani ya Somalia

Vifo vya watu 2 kati ya 100 walioambukizwa, vinatarajiwa.

Reuters inasema kuwa vifo 533 kutokana na cholera au kuhara vimerekodiwa kufikia sasa.

Chanzo cha picha, WHO

Maelezo ya picha,

Kunywa maji chafu ni chanzo kikuu cha vifo vingi duniani

Shirika la WHO limekuwa likiandika leo kwenye mtandao wake wa kijamii wa Twiter kuhusiana na hatari ya kunywa maji chafu, huku likisema kuwa, inawauwa watu wengi sana kote duniani kila mwaka.