Arsenal yawatungua Boro 2-1

Arsene Wenger ajitoa kimaso maso kwa kuwabandua Middlesbrough
Maelezo ya picha,

Arsene Wenger ajitoa kimaso maso kwa kuwabandua Middlesbrough

Hatimaye usiku wa kuamkia leo Arsenal imejitoa kimaso maso baada ya kuwatungua Middlesbrough bao mbili kwa moja.

Mchezo huo ulianza polepole huku kila timu ikiangalia mwanya mpaka dakika chache kabla ya mapumziko free-kick ya Alexis Sanchez ilipowanyanyua kwenye viti mashabiki wa Arsenal.

Middlesbrough wakalipiza kisasi mara tu baada ya kuanza kipindi cha pili pale ambapo Alvaro Negredo alipoitupia ndani cross ya Sterwart Downing. Hata hivyo Arsenal ilikuwa inazihitaji sana pointi tatu kwa hivyo Mesut Ozil akaokoa jahazi kwa kutupia lingine.